Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Akizungumza katika kongamano la maadhimisho ya kuzaliwa Imam Mahdi (aj) sambamba na kumbukumbu ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, lillyofanyika katika Ukumbi wa Jamiatul Mustwafa, uliopo jijini Daresalam mtaa wa Kigamboni, Sheikh Jalala alisisitiza kwamba; Uislamu ambao umeshikama na utamaduni wa Karbala ni Uislamu ambao unapambania dhulma na kusimamia haki.
Sheikh Hemedi Jalala alianza khutuba yake na maneno ya Mwenyezimugu kwa kusoma aya Tukufu ya Qur’an isemayo:
"كَتَبَ اللَّهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ"
Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.
(Surat Almujadial: 21)
Baada ya kusoma aya hiyo ambayo inaelezea ahadi ya Mwenyezi Mungu kuhusu ushindi wa haki juu ya batili alielezea siri ya Ushindi wa Kiislamu huku kifafanua maana ya Aya hiyo, alisema kuwa: Uislamu una siri kadhaa za ushindi, ikiwemo: Kuishi kwa mujibu wa vitendo na mafunzo ya Imam Hussein (a.s), na kuamini uwepo wa Imam Mahdi (atfs) ikiwa ni njia ya matumaini ya kusimamishwa haki na uadilifu duniani.
Kiongozi huyo wa Mashia Tanzania, akiwa naendelea na khutuba yake aliongeza kusema kuwa: Uwepo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni sehemu kubwa ya ushindi wa Uislamu, kwani ndio dola pekee inayotetea Uislamu wa hekima na uongozi wa kweli ilioasisiwa na Imam Khomeini (ra) na kuendelezwa na Kiongozi wa Mapinduzi, Sayyid Ali Khamenei (Mola amuhifadh).
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Mashia Tanzania alisisitiza kwamba: Uislamu sio dini ya udhalili bali ni dini iliyojaa heshima. Akirejea kauli ya Imam Hussein (a.s), isemayao: "هيهات منا الذلة"
(Uwe mbali nasi udhalili), alisema kuwa: Uislamu unakataa kuwanyenyekea madhalimu na unahimiza kuishi maisha ya heshima, ujasiri na kupambana dhidi ya dhulma kwa misingi inayo fuata haki na uadlifu.
Aliongeza kwa kusema kwamba: Uislamu uliobeba siasa ya Karbala, ndio Uislamu unaotambua adui, unapambana naye, na kuhakikisha haki na uadilifu vinatawala duniani.”
Uongozi na Mustakabali wa Umma
Katika mwendelezo wa khutuba yake alisema kuwa: Nguvu ya Uislamu inatokana na uwepo wa: Uongozi thabiti wa Kiislamu, wanazuoni na marjaiya na naibu wa Imam wa Zama. Alisema kuwa: uongozi huo ndio ambao unautuliza Umma hata katika nyakati ngumu na kuwapa matumaini ya ushindi.
Alisema kwamba: Uislamu unao shikama na itikadi hii hautetereki, kwa sababu una amini kwamba, dhulma itaondoka na haki itatawala. Uislamu ni ushindi, izza na utukufu.”
Kongamano hilo pua lilihudhuriwa na masheikh mbalimbali nchini humo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuia ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Dr. Sheikh Al-Had Mussa Salum, Mwenyeji na mwandalizi wa hafla hiyo Dkt, Ali Taqawi pamoja na waumini kutoka maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.
Sheikh mkuu wa Jumuiya ya Mashia Tanzania alihitimisha khutuba yake kwa kuwataka Waislamu kushikamana na Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kuishi kwa mujibu wa thaqafa na utamadubi wa Karbala ya Imam Hussein (a.s), ili Umma uendelee kusonga mbele huku ukiwa umebeba heshima na nguvu.



Maoni yako